Ligi Kuu

Simba yaishindilia Mtibwa, Ndemla ashangaza!

Sambaza....

Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mbele ya Wakata Miwa Mtibwa Sugar katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijni Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa raundi ya 28 Simba wakicheza kandanda safi kabisa huku pia wakiutumia kumuaga mlinzi wao wa kati Pascal Wawa ambae amedumu Msimbazi kwa miaka minne.

Wawa akitimiza majukumu ya mwisho katika mchezo wake wa mwisho wakuwatumikia wekundu wa Msimbazi Simba (picha na Lilian Mukulu)

Magoli ya Simba yalipatikana katika dakika ya 17 na 44 kupitia kwa Sakho na goli la kujifunga la Shaban Kado. Sakho alifunga bao la kwanza baada ya kugongeana vyema na Kibu kisha kuwatambuka walinzi wa Mtibwa na kufunga kirahisi. Goli la pili ni kama zawadi vile kutoka kwa Shaban Kado baada ya kuudaka mpira mwepesi wa Peter Banda kizembe na kuutumbukiza wavuni.

Katika hali ya kushangaza kiungo wa Simba anaeitumikia Mtibwa Sugar kwa mkopo alitolewa nje ya uwanja katika kipindi cha pili baada ya kuonyesha kadi nyekundu kwa kosa la kumkanyaga makusudi Sadio Kanoute akiwa hana mpira.

Said Ndemla

Kwa kadi hiyo aliyoipata katika dakika ya 68 Ndemla sasa ataikosa michezo miwili ya Mtibwa Sugar iliyobaki ukiwepo mmoja dhidi ya Yanga utakaopigwa Jijini Dar es salaam pia.

Kwa matokea hayo bado yanaiacha Mtibwa Sugar katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 31 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.