Ligi Kuu

Simba yamthibiti mbabe wa Yanga!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuifunga  KMC katika mchezo wa kirafiki wa kujipima uwezo uliofanyika katika uwanja wa Simba-Mo Arena Bunju jijini Dar es salaam.

Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi wa soka  ulipigwa majira ya jioni huku ukishuhudiwa na vituko mbalimbali kutoka kwa mshabiki walioonekana  “wamelimiss” kandanda.

Charles Illanfia alikua wakwanza kuiandikia bao KMC katika dakika ya 32 kabla ya nahodha John Bocco kuchomoa dakika ya 35 baada ya shuti la Pascal Wawa kubaki likizagaa langoni mwa KMC na hivyo kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao moja kwa moja.

John Bocco akifunga mbele ya mlinda mlango  Juma Kaseja na mlinzi Ismail Gambo.

Kipindi cha pili Simba waliongeza mabao mawili kupitia kwa John Bocco na Ibrahim Ajib aliefunga bao la kideoni dakika za jioni kabisa na kuufanya mchezo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao matatu dhidi ya moja la KMC.

Kmc kabla ya mchezo wa leo ilicheza pia na Yanga mchezo wa kirafiki na kushinda mabao matatu kwa sifuri.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.