Stori

Simba yapata mamilioni mengine kwenye soka la vijana

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wameingia makubaliano ya kukuza na kuendeleza soka la vijana na kampuni ya MobiAd leo Jijini Dar es salaam.

Mkataba huo wa miaka miwili wenye thamani ya milioni 500 umesainiwa na Watendaji wakuu wa pande zote mbili mbele ya waandishi wa habari huku kila upande ukishukuru na kuahidu kutumia nafasi hiyo ipasavyo.

 

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema ili Simba wawe na timu bora ni lazima kuwe na maandalizi kwa vijana kama ambavyo baadhi ya wachezaji walipita katika timu za vijana.

Imani Kajuna “Ili tuwe na timu bora zaidi ya wakubwa ni lazime uwe na timu imara zaidi ya vijana. Na ili uwe na timu imara ya vijana ni lazima uwekeze sana katika vijana hawa.
Mfano Mohamed Hussein “Tshabalala” na John  Bocco hawa ni wachezaji ambao watu waliwekeza tangu wakiwa wadogo na leo tunaona matunda yake.”

Imani Kajula amesema kupitia udhamini huo watafikia vijana wote nchini Tanzania wenye vipaji ili kuweza kuwaendeleza na kuwatumia hapo baadae.

Imani Kajula Mtendaji mkuu wa Simba Sc

“Tutafika katika kila eneo kila kitongoji cha hii nchi ili kuweza kupata vijana wenye vipaji. Tutawatafuta nchi nzima na kuwaleta vijana pamoja, tunataka tupate vijana ambao wanaipenda Simba halafu ndio tutawaingiza kwenye mfumo wa Simba ili waweze kuitumikia Simba,” alisema Imani Kajula.

Nae mtendaji mkuu wa kampumi ya MobiAd amesema  maandalizi kwaajili ya Taifa la kesho ni vyema yakaanza mapema lakini pia ametaja kiasi cha udhamini ambacho watakitoa kwa Simba.

“Mara nyingi tunasikia vijana ndio Taifa la kesho lakini maandalizi yanatakiwa yaanze mapema ili kufanikisha utayari huo wa vijana. Tunaanzisha safari ya kuwaunga mkono vijana wenzetu, tunajua hii safari ni ndefu lakini tunamini tutafanikiwa.

Mtendaji mkuu wa MobiAd Rushimo Shikonyi.

Tunatangaza udhamimi kwa Simba na moja kwa moja katika soka la vijana na kwa kuanzia tuu tutatoa milioni 500 miaka miwili hii na tunaamini tutaendelea mbele zaidi.
Tuna mategemeo makubwa sana na huu uwekezaji tunamini vijana watafaidika katika hili.” alisema Rumisho Shikonyi Mtendaji mkuu wa MobiAd.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli maarufu hapa Jijini alihudhuriwa pia na manahodha wa Simba Mohamed Hussein na John Bocco ambao pia waliandamana na makocha na viongozi wa benchi la ufundi la Simba kina Mussa Mgosi, Nicco Kiondo na Patrick Rweyemamu

 

Sambaza....