Walinzi wa kati wa Coastal Union Ibrahim Ame "Varane" na Bakari Mwamunyeto
Tetesi

Simba yavamia Coastal yambeba pacha wa Mwamunyeto!

Sambaza....

Harakati za usajili zinaendelea haswa vilabu vikongwe vya Simba na Yanga kwa vilabu kuendelea kujiimarisha baada ya usajili kufunguliwa rasmi August 1 na kufungwa August 31.

Baada ya Simba kumkosa Bakari Nondo Mwamunyeto kutokana na jeuri ya pesa ya GSM na kupelekea Mwamunyeto kumwaga wino Yanga sasa Simba imerudi tena Coastal Union na kubeba kitasa kingine.

Bakari Nondo, Ibrahim Ame, Soud Dondola.

Ibrahim Ame wakati wowote atatambulishwa na Wekundu wa Msimbazi Simba kama mlinzi wao mpya baada ya kumkosa Bakari Mwamunyeto.

Ame maarufu kama Varane anasifika kwa umbo lake kubwa lililojengeka, utulivu na uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya juu. Katika Msimu huu uliomalizika  yeye na Mwamunyeto wa walikua na pacha nzuri na kupelekea Coastal Union kutoka na “cleansheet” 13.

Sambaza....