Sambaza....

Moja kati ya wachezaji wa Tanzania wenye profile kubwa hapa Nchini basi ni Simon Msuva, ukitaja majina matano ya wachezaji wa ndani ambao ni mfano wa kuigwa na wengi hapa nchini huwezi kusahau jina lake.

Muda wa dirisha la usajili ndio huu na tayari tetesi zipo kuhusishwa kuelekea Kariakoo yaani Simba na  Young Africans lakini dili halijafanikiwa! Ni tetesi na itabaki kuwa hivyo mpaka itakapokuwa rasmi.

 

Vizuri! Ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kupata nafasi ndani ya timu zote mbili na akaingia kikosini moja kwa moja lakini jicho lake naona lipo nje ya Nchi zaidi, labda kama itawekwa pesa nzuri ambayo itamvutia ijapo bado ni mapema sana.

Young Africans kuna wachezaji wapya na wale waliokuwepo ambao wanacheza pembeni wanaoweza kutoa huduma bora tu katika eneo analocheza Simon Msuva mfano Nzengeli, Moloko na Skudu ijapo madaraja yao yanatofautiana.

Simom Msuva akimtambuka mlinzi wa Niger

Simba pia wapo wachezaji wengi ambao wanacheza eneo hilo na wanaweza kuipa timu kitu bora ndani ya uwanja kama Onana, Luis, Kibu au hata Saidoo na Phiri ambao wanaweza kucheza eneo hili kwa aina ya mfumo wa Robertinho.

Binafsi sioni uhitaji wa Simon Msuva sana ndani ya Klabu hizi mbili kwa kuzingatia ubora wa timu zao, wachezaji waliopo na mbinu za Walimu japokuwa anaweza kwenda na kupata nafasi moja kwa moja pale Simba na Young Africans.

Simon Msuva.

Rahisi. Bado miguu yake ina kitu kikubwa cha kutoa nje ya nchi zaidi kuliko hapa ndani ambapo itapendeza yeye kuja kumalizia soka japokuwa pembeni ya yote kuna kitu kinaitwa pesa ambayo inaweza kumfanya akacheza Tanzania pia.

Himid Mao, Mbwana Samatta, Abdi Banda hata Novatus Dismas ambaye hana muda mrefu ametoka nje wanafanya vizuri sana hivyo bado tunahitaji kitu cha tofauti kutoka nje zaidi kwa Simon Msuva.

Mwisho wa yote pesa ndio inazungumza na Simon Msuva maisha ya mpira ni ajira kwa wachezaji wetu! Lengo ni kupata pesa, hivyo kama dau litakuwa zuri basi dili litakamilika kama ikiwa maslahi ndio kipaumbele namba moja kwake.

 

Sambaza....