Blog

Sishoboki kwa Haji Manara- NUGAZ

Sambaza....

Yanga imeshatoka kwenye michuano ya kombe la mapinduzi, inarudi tena Tanzania bara kupambana kwa ajili ya ligi kuu Tanzania bara pamoja na kombe la shirikisho.

Jumatatu Simba itakuwa inacheza na Mtibwa Sugar kwenye fainali ya kombe la mapinduzi. Timu zote zimeingia fainali Baada ya kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Simba iliifunga Azam FC wakati Mtibwa waliwatoa Yanga kwenye michezo ya nusu fainali. Baada ya kutoka kwenye michuano hii , Afisa Mhamasishaji wa Yanga alisema michuano hii ni midogo kwao.

Kauli ambayo ilipingwa vikali na Haji Manara ambaye alidai Antonio Nugaz ameidharirisha michuano hii kwa kuiita michuano midogo.

Leo kupitia ukurasa wa Instagram wa Antonio Nugaz alipost video ambayo ilikuwa inaelezea maandalizi ya Yanga kwenye michezo mbalimbali aliyokuwa anahojiwa na kituo cha Azam TV.

Kwenye comment kuna shabiki aliandika kwa kumsifia Antonio Nugaz na kumwambia yeye ni sawa na vichwa 100 vya Haji Manara.

Antonio Nugaz aliijibu comment ile kwa kuandika kuwa “hakika afu sina shobo , sishobokei hawawezi kupost bila kunitaja”- alimalizia kuandika hivo Afisa mhamasishaji huyo wa Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.