Wachezaji wa Taifa Stars
AFCON

Taifa Stars: Tunaitaka Afcon ya Ivory Coast.

Sambaza....

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tayari kipo nchini Tunisia kikifanya maandalizi ya mwisho kabisa kuelekea mchezo wa mwisho wa kufuzu Afcon dhidi ya Algeria ugenini.

Stars ipo nchini humo ikilenga kupata kambi sahihi inayoendana na hali ya hewa ya nchini Algeria ambapo Tanzania inatafuta historia yakufuzu michuano ya Afcon kwa mara ya tatu.

Akiongea na tovuti ya Kandanda.co.tz moja kwa moja kutoka nchini Algeria msemaji wa Shirikisho la soka nchini TFF Cliford Marion Ndimbo amesema “Tayari wachezaji wameendelea kuripoti kambini na kesho kikosi kinatarajia kuondoka hapa Tunisia na kuelekea nchini Algeria ambapo ndio tutachezea mchezo huo,” alisema Ndimbo na kuongeza;

Wachezani wa Tanzania “Taifa Stars” wakishangilia

“Hali ya kikosi ipo vizuri na kikosi kina morali kuelekea mchezo huo na kila mmoja anatamani mchezo huo ufike maana nia ni kufanya vizuri.”

“Kila mmoja anazingumzia Afcon kwamba kila wanataka tufuzu kwa mara nyingine, hii ndio nia ya dhati ya TFF, benchi la ufundi lakini pia nia ya mdau namba moja ambae ni serikali. Nia ya dhati ni kuhakikisha tunafuzu kucheza Afcon kwa mara nyingine tena,” alimalizia Ndimbo

Stars watashuka dimbani nchini Algeria kusaka alama moja tu ambayo itawafanya kufuzu katika kundi hilo sambamba na Algeria na kuwaacha Uganda na Niger.

Stars ina alama saba ikishika nafasi ya pili nyuma ya Algeria waliofuzu tayari wakati Uganda wana alama nne wakishika nafasi ya tatu. Ni alama moja pekee ndio itakayoipeleka Stars Afcon bila kujali matokeo ya Uganda na Niger.


Sambaza....