Sambaza....

Simba Sc inakaribia kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara huku baada ya kuukosa takribani miaka mitano wakisaliwa  na michezo mitatu pekee wakihitaji alama mbili tuu.

Wamebakiwa na michezo miwili ugenini (dhidi ya Singida utd na Majimaji ya Songea) na mchezo mmoja nyumbani dhidi ya Kagera Sugar.

Mpira wa kisasa wanasema unahitaji pesa, naam na ndio kitu walichokifanya Wekundu wa Msimbazi msimu huu. Tangu usajili wao na hata uendeshaji wa timu wa Sasa  Simba imeonekana kuwekeza kwelii na sasa inaelekea kupata matunda ya uwekezaji wao.

Katika usajili wao wa msimu huu walichukua wachezaji waandamizi wa Azam fc waliionekana kama wamemaliza muda wao pale Chamanzi hivyo hawana lolote tena.

Hii kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na será yao mpya ya Azam ya kuwatumia vijana, na kuamua kuachana na wachezaji wakongwe. Na hiki ndio kwa kiasi kikubwa kilipelekea uimara wa kikosi cha ubingwa cha Wekundu wa Msimbazi msimu huu.  John Bocco, Aishi Manula, Erasto Edward Nyoni na Shomary Kapombe wote kwa wakati mmoja walitoka Azam fc na kujiunga na Simba Sc .

Tovuti yako pendwa ya kandanda.com inakuletea mchango wa wachezaji hão wa zamani wa Azam jinsi walivyoipa ubingwa Simba Sc .

Erasto Edward Nyoni

Moja ya nguzo muhimu katika eneo la ulinzi wa Simba msimu huu. Ameweza kucheza sehemu zote katika eneo la ulinzi. Ameweza kumudu kucheza kama beki wa pembeni (kulia na kushoto) beki wa kati na kiungo wa ulinzi.

Mbali na kuweza kucheza vizuri nafasi ya ulinzi pia ameto mchango mkubwa katika upatikanaji wa mabao. Amekua akifunga pia akitoa msaada wa mabao. Amefunga magoli matatu mpaka sasa katika VPL.

Moja ya mabao yake muhimu na yaliyoifaidisha Simba msimu huu ni pale alipofunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Yanga April 29 na kuipa ushindi timu yake.

Shomari Kapombe

Ni kama amerudi nyumbani baada ya kwenda Ufaransa na baadae kurudi nchini kujiunga na AzamFc na baadae msimu huu akajiunga na Simba.

Alikosa nusu msimu baada ya kuumia alikua na timu ya Taifa. Lakini aliporudi alikua imara na kuzidi kuimarisha timu katika eneo la ulinzi na kiungo. Kocha Mfaransa mara nyingi amekua akimtumia kama kiungo wa ushambuliaji kutoka na uwezo wake wa kucheza popote uwanjani.

Mpaka sasa ametoa pasi nne za mabao katika VPL. Moja ya pasi zake muhimu za mwisho alizotoa ni katika mchezo dhidi ya Ndanda ambapo Emmanuel Okwi alifunga bao pekee katika mchezo huo.

Aishi Salum Manula

Kipa bora wa nchi kwa miaka miwili mfululizo na kipa namba moja wa Timu ya Taifa. Hakika hapa Simba walifanya usajili muhimu na makini kabisa.

Amekua imara katika lango lake na katika kuipanga timu yake pindi Simba inaposhambuliwa. Achana na kile alichokifanya katika mchezo wa ugenini dhidi ya Almasry kule Misri. Wana Simba watamkubuka jinsi alivyoweza kucheza vizuri katika lango katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar (Jamuhuri Morogoro) na katika mechi dhidi ya Yanga katika raundi ya kwanza (Uhuru Stadium).

Hueda akatwaa tena tuzo ya kipa bora msimu huu na kueka rekodi ya kuichukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo.

John Raphael Bocco!

Mr Captain unaweza kumuita, achana na mabao yake aliyohama nayo Azam na kuyaleta Simba tazama jinsi alivyokua kiongozi imara na muhamasishaji wa ndani na nje uwanja.

Simba kwa kumsajili John Bocco ni kama wamepata mshambuliaji pia kiongozi katika timu. Mpaka sasa ana mabao 14 katika Ligi Kuu Bara na kua namba mbili katika orodha ya wafungaji bora nyuma ya Emmanuel Okwi.

Baada ya kuipa ubingwa, pia Simba Sc inamtegemea kua moja ya wachezaji muhimu katika harakati zake za michuano ya Kimataifa msimu ujao.

Sambaza....