Blog

TFF yakataa michezo ya Simba na Yanga!

Sambaza....

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limepiga marufuku michezo ya kirafiki inayochezwa haswa na timu za Dar es salaam kutokana na kutokufuata utaratibu wa wizara.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa na msemaji wake Cliford Marion Ndimbo imezitaka klabu zote kutokucheza mchezo wowote bila kutoa taarifa katika Shirikisho la Soka.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya TFF!

Timu za Transit Camp, Azam fc, KMC, Simba na Yanga zote zimeitwa TFF kutokana na kucheza michezo ya kirafiki huku pia wakikiuka miiko ys wizara ya Afya na wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusiana na ugonjwa wa covid 19.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.