Papy Kabamba Tshishimbi.
Tetesi

Tshishimbi arudisha pesa za GSM

Sambaza....

Bado sakata la Papy Kabamba Tshishimbi na klabu yake ya Yanga linazidi kupamba moto. Nahodha huyo wa Yanga mkataba wake unaisha mwezi huu na hakuna taarifa sahihi ya yeye kuongeza mkataba mpya na klabu yake hiyo.

Wiki hii kaimu katibu mkuu wa Yanga , Patrick Saimon alidai kuwa wamempa Papy Kabamba Tshishimbi siku kumi na nne kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo tofauti na hapo wataachana naye.

Awali inasemekana kuwa klabu ya Yanga na nahodha wao Papy Kabamba Tshishimbi walifikia makubaliano ambayo kwa wakati huo yaliambatana na kiasi fulani cha pesa ambacho ni kama kishika uchumba.

Papy Kabamba Tshishimbi.

Baada ya kauli hiyo ya kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga , Patrick Saimon kauli ambayo ilionekana kumuudhi nahodha huyo wa Yanga , inasemekana nahodha huyo ameamua kurudisha kiasi kile ambacho Yanga ilitoa kama kishika uchumba.

Habari za uhakika kutoka Yanga zinadai kuwa Nahodha wa kikosi hicho Papy Tshishimbi Leo amerejesha fedha dola 30,000 (Milioni 69) za Klabu ya Yanga ambazo aliwekewa kwenye akaunti yake Kama Ada ya Usajili. Papy amedai kuwa Kama Yanga wanataka asaini mkataba wa miaka miwili wampe dola 50,000 (Milioni 116 za Kitanzania) na mshahara wa milioni 12 kwa mwezi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.