Papy Kabamba Tshishimbi.
Tetesi

Tshishimbi: Sijasajiliwa As Vita.

Sambaza....

Jana kulitokea habari za usajili wa aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya Yanga , Papy Kabamba Tshishimbi kusajiliwa na As Vita ya nchini Congo.

Papy Kabamba Tshishimbi amedai kuwa kwa sasa wako kwenye mazungumzo na As Vita na muda wowote wanaweza wakaingia kwenye mkataba mpya na As Vita.

“Bado sijasajiliwa na As Vita ila tuko kwenye mazungumzo na As Vita. Mazungumzo ambayo yanaweza kumalizika na kusajiliwa na As Vita”- alisema Papy Kabamba Tshishimbi.

Papy Kabamba Tshishimbi alishindwa kuongeza mkataba na Yanga kutokana na kutokukubaliana kila pande hivo akaamua kurudi kwao Congo.

Sambaza....