Ligi Kuu

Tulipuliziwa dawa vyumbani- NAMUNGO

Sambaza....

Moja ya mechi kali ya ligi kuu Tanzania bara ilichezwa jana kwenye uwanja wa Taifa ambapo Simba iliifunga Namungo FC  magoli 3-2. Namungo FC walionesha ushindani mkubwa kwenye mechi hii.

Baada ya mechi hii kocha mkuu wa Namungo FC alidai kuwa wao walikuja kushindana kwenye mechi ndiyo maana idadi kubwa ya magoli ilipatikana.

“Sisi hatukuja kuzuia kwenye hii mechi , sisi tulikuja kushindana kwenye mechi hii , ndiyo maana idadi ya magoli imekuwa kubwa kiasi hiki”.

Alipoulizwa kama goli la tatu lilikuwa offside alidai kuwa anadhani lilikuwa offside lakini atajiridhisha kwenye TV.

“Nadhani goli la tatu la Simba lilikuwa offside lakini tutajaribu kuangalia kwenye TV ili kujiridhisha zaidi kama ilikuwa Offside au hapana”.

Kuhusu timu ya Namuongo FC kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko, alidai kuwa chumba kilikuwa na hewa nzito.

“Tulitoka nje ya vyumba kupata hewa safi. Hakukuwepo na hewa nzuri ndiyo maana tulitoka nje , hewa ilikuwa nzito kama kumepuliziwa vitu “alimalizia Kocha huyo wa Namungo FC

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.