Mabingwa Afrika

Tunaenda kwa ajili ya kufuzu nusu fainali- Aussems

Sambaza kwa marafiki....

Haya ni maneno ya kocha mkuu wa Simba ambaye alikuwa anazungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz jana kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe.

Kocha huyo wa Simba ameendelea kuamini kuwa Simba inaenda kwa ajili ya kufuzu hatua ƴya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Wana nafasi ya kufanya hivo. Na kocha huyo anaamini wana uwezo mkubwa wa kufanya hivo na wanaenda Congo kwa ajili ya kupigana ili wafuzu hatua ya nusu fainali.

Simba inahitaji kupata sare ya magoli au ushindi wa aina yoyote kwenye mechi ya marudiano . Matokeo ambayo yatamfanya aweze kufuzu moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz