Tetesi

Ugomvi mzito kati ya YONDANI na LUC EYMAEL

Sambaza....

Kelvin Yondani na Luc Eymael hawapatani !Kuna ugomvi wa ndani Kati ya Kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael na beki mkongwe wa Yanga Kelvin Yondani. Ugomvi huu umeanza baada ya mechi ya Yanga na Kagera Sugar.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Kagera Sugar kushinda goli 3-0 , kwa mujibu wa vyanzo vya ndani , Kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael hakuridhika na viwango vya baadhi ya wachezaji wa Yanga akiwemo Kelvin Yondani .

Hali hii ilisababisha hali ya kutoelewana kati yao, ikafikia hatua Kelvin Yondani akawa haendi au kuchelewa mazoezi. Kocha wa Yanga aliamua kutomwanzisha Kelvin Yondani.

Tangu mechi ya Kagera Sugar na Yanga , Kelvin Yondani hajapewa nafasi kwenye kikosi cha Yanga . Luc Eymael amekuwa akimpa nafasi kubwa sana ndani ya kikosi Saidi Juma Makapu ambaye amekuwa akicheza na Lamine Moro.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.