Ligi Kuu

Wachezaji wa Simba hawajui thamani ya jezi ya Simba, Wanakera sana- HAJI MANARA

Sambaza....

 

Mara Baada ya Simba kutoka sare ya magoli mawili kwa mawili , matokeo ambayo wengi hawajapendezwa nayo kutokana na kuwa na imani ya wao kuifunga Yanga , msemaji wa Simba Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram amedai wachezaji wa Simba hawajui thamani ya jezi yao.

“Lau wachezaji wetu mngekumbuka maneno ya huyu tajiri Siku ya mchezo jana, hizi tambo za kupata draw zisingekuwepo. Wenzetu hawapati mnachokipata , wanaoenda daladala mpaka Mbeya, hawakai camp nzuri , hawalipwi kwa wakati, hawapati bonus mzipatazo lakini wanawazidi fighting spirit na commitment kwa mbali sana

“Bado thamani ya jezi kwa baadhi ya wachezaji wetu mnaiangusha sana, kweli mpira una matokeo matatu ila kwa jana ile sare haikustahili kwa ukubwa wa Simba, mmewaangusha sana mashabiki wetu ambao always wanakuja kuwapa nguvu

Mashabiki wa Simba Sc

Mimi binafsi najiuliza nitakuwa nayo legitimacy ya kuwaita mashabiki uwanjani? ,bodi yetu makini mmeiangusha, management tumelowa kabisa ,na mnampa wakati mgumu tajiri anayeweka pesa zake , kifupi baadhi yenu mmeboa mno”. Alimalizia kuandika hivo , yapi maoni yako Haji Manara anastahili kuwatupia lawama mashabiki ?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.