Ligi Kuu

Wachezaji YANGA kupewa Gari kila mmoja

Sambaza....

Pamoja na kwamba hali ndani ya klabu inaonekana ni hali Mbaya kiuchumi kutokana na madeni mengi ambayo Yanga inadaiwa na wachezaji . Wachezaji wanadai mishahara pamoja na ada ya uhamisho lakini wamejinasibu kuwanunulia magari wachezaji wao wote.

“Sasa hivi tunataka kuanzisha darasa la BRANDING kwa wachezaji wetu hasa hasa hawa wa ndani ambao wanaonekana wametoka uswahili “- alianza kwa kusema hivo Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz.

“Tunataka tuwafunze jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii , jinsi ya kupost vitu ambavyo vinaweza kuwa na faida kwao , wanatakiwa kujua wao ni wachezaji wenye nguvu kwenye jamii neno ambalo wataliandika kwenye mitandao ya kijamii linaweza kuleta madhara hasi na chanya”.

“Hata namna ya kula mbele ya watu tunataka tuwafundishe , kama nilivyosema hawa wachezaji wametokea uswahili kwa hiyo hawajui hata namna ya kula mbele ya jamii ili kulinda chapa yao”.

“Nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja ambaye ni anauza magari tuone uwezekano wa sisi kuwakopesha wachezaji Athlete Crown kila mmoja ambapo watakuwa wanakatwa kwenye mishahara , hata mchezaji akitaka aina fulani ya gari iwe prado au nyingine anakuwa huru kuchagua”. Alimalizia kusema Afisa mhamasishaji huyo wa Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.