Mashindano

Yanga haina shida na mataji madogo- NUGAZ

Sambaza kwa marafiki....

Jana kulikuwa na nusu fainali ya kombe la mapinduzi kati ya Mtibwa Sugar na Yanga . Mechi ambayo ilimalizika kwa Mtibwa Sugar kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti (4-2) Baada ya kutoka sare ya (1-1) kwenye muda wa kawaida.

Baada ya mechi hiyo Afisa Mhamasishaji wa Yanga , Antonio Nugaz amedai kuwa Yanga haikuwa na shida na vikombe vidogo kama mapinduzi.“Wameshinda wameingia fainali , ila Yanga haina shida na vikombe vidogo dogo kwa sasa watatuumizia wachezaji wetu”-amedai Afisa huyo mhamasishaji wa Yanga.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz