Blog

Safari hii Yanga itampita mtani wake, Simba itapotezwa vibaya.

Sambaza....

Kuna ukweli ambao mashabiki wa Simba hawatokuwa tayari kuusikia. Ukweli ambao utaonekana ni mchungu sana kama ukitokea kwenye macho yao ya nyama.

Ukweli huu ulianzia kwenye matamasha. Matamasha ya Simba Day pamoja na lile tamasha la wiki ya mwanachi ambalo linamilikiwa na Yanga.

Yanga inaongozwa na watu makini katika masuala ya kifedha, Arafat Haji (pichani) ni moja kati ya timu hiyo

Matamasha haya yalikuwa ya klabu kubwa hapa nchini. Klabu ambazo zinaushindani sana hapa nchini na ndizo klabu ambazo zina mashabiki wengi nchini.

Sarpong akishangilia bao

Swali kubwa lilibaki ni nani ambaye anaweza akafanya vyema kwenye haya matamasha? Wote tulisubiri jibu sahihi. Yanga walifanya vyema kuzidi Simba.

Tunakataa ukweli kuwa pamoja na watu kujaza au kutojaza uwanja mpangilio wa Tamasha ilikuwaje ? Hapa ndipo ubora wa tamasha la Yanga unapoanzia.

Duka la Yanga

Attention ya Tamasha ilianzia pale Mashabiki wa Yanga kuwapokea wachezaji wao kwa aina ile ya kujazana uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hakuna ambae hakutaka kuwaona Tuisila , Tonombe , Sarpong , Carlos walichonacho hata ambao hawakuenda uwanjani walikaa majumbani kusubiri kuona .

Hapa utaona ile attention ya kuwa tumesajiri mchezaji ambae Yanga walimtaka haikuoata mailage Kama kwenda uwanja wa ndege na kupokea mchezaji kwa maandamano .

Harmonize

Pili uwepo wa Konde boy(Harmonize) baada ya Almasi(Diamond) ilikuwa alama nyingine kuona nini kitafanyika .

Kizuri Sana viongozi wa Yanga yote haya wakayajua na kuandaa mpangilio sahihi na ndio maana unaona hata ilikuwa rahisi kwa MCs kwendesha Tamasha kiurahisi kwa maana ya kiu ya kuona ilikuwa upande wa mashabiki yaani Wananchi .

Ukikumbuka hata Haji Manara alisema hatafanya promotion kubwa kwa kuwa mashabiki wa Simba walikuwa wanajua umhm wao , hapa utajiuliza kwanini kuna advertising and exhibitions kila siku in business ?

Manara

Tatizo moja kubwa watu wanaogopa kuwaambia Simba kuwa wameona wamefika kwenye optimal point na wamerelax na hii ni mbaya ila kwa kilichofanyika Jana kinawaamusha viongozi na mashabiki wa Simba kutoka usingizini ndio maana hawajadili hoja sasa ila ushabiki .

HII ITAKUWA MBAYA SANA IKIJA KUTOKEA MFUMO WA MABADILIKO WA YANGA UKAWA BORA KULINGANA NA WAKATI NA UKALETA TIJA .

Nilishawahi kusema kuwa YANGA Wana nafasi ya kuwatesa Simba miaka mingi Kama tu watakuja na mfumo sahihi na kila kitu kikawa Kama mfumo unavyotaka na upande wa Simba Kuna kitu kitakuja kutokea kutoka kwa mashabiki .

Wajuzi wengi wa theoris of Investment Mara nyingi tulisema Kuna UKUTA .

Lakini kiuwezo na kiufundi ndani ya uwanja hakuna Kama SIMBA hapa Tanzania kwa mafanikio , display ya timu , wachezaji na competition Kati ya wachezaji ila sio kwamba wengine hawawezi kufanya zaidi au kuwa na timu nzuri zaidi Ni suala la kujipanga tu .

Senzo

Lakini kama Yanga wakikaa na kutulia wanaweza wanatengeneza mfumo bora dhidi ya Simba na kuwazidi Simba. Jana wameonesha picha za duka lao la jezi.

Kitu hiki ni kipya hapa nchini kwa timu kuwa na duka lake la jezi. Ni mabadiliko ambayo yanafanyika taratibu na yanaweza yakawafanya Yanga kuwazidi Simba ambao walitangulia kuanza mabadiliko.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.