Tetesi

YANGA kumleta Mshambuliaji zaidi ya KAGERE !

Sambaza....

Baada ya Yanga kushindwa kumnasa kiungo hatari wa UD Songo Luis Jose Misquissone kutokana na dau kubwa, mchezaji huyo alitaka shilingi milioni 110 za kitanzania kama ada ya uhamisho, Yanga imehamia mashambulizi yake kwa Dickson Ambundo.

Mchezaji huyo anayekipiga Gor Mahia kwa sasa amewahi kucheza Alliance FC ya Mwanza msimu juzi , msimu ambao alifanya vizuri akiwa na Alliance FC kwa kufunga magoli zaidi ya 10 kwenye msimu huo.

Mafanikio hayo makubwa yaliwavutia Gor Mahia kumsajili msimu jana , na kwa sasa Yanga imepanga kumrudisha mchezaji huyo hatari ambaye hucheza kama winger wa pembeni. Pia Dickson Ambundo anauwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa pili.

 

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.