Ligi Kuu

Yanga na Namungo ni vita ndani ya vita kwa Mkapa.

Sambaza....

Nje ya vita vya timu kugombea alama tatu muhimu kwa ajili ya kujiimarisha katika msimamo wa ligi kuu, naviona vita vingine ndani ya vita hivi ambayo ni mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora.

Mfungaji bora wa ligi ya NBC hadi sasa ni Fiston Mayele mwenye goli 11 hadi sasa huku akifuatiwa na mzawa Reliant Lusajo mwenye magoli 10. 

Mechi ya leo inakwenda kuwakutanisha vinara hawa wenyewe kwa wenyewe, ambaye moja     ( Mayele) yupo kwenye trend nzuri ya ufungaji kwa maana ya kufunga mfululizo huku Lusajo akiwa kama kasimama ni muda sasa hajafunga.

Fiston Kalala Mayele.

Huenda akaamka leo dhidi ya timu yake ya zamani ya Yanga ambayo alipata kuitumikia huko nyuma, huku mwenzake Mayele akitazamiwa kuendeleza kupachika magoli na kutetema kama kawaida yake.

Nilipata kumsikia akisema ana deni kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kutowafunga baadhi ya timu ikiwemo Namungo huwenda leo akataka kutimiza hilo.

Mshambuliaji wa Namungo Reliant Lusajo akikokota mpira mbele ya Abdulrahmani Mussa wa Ruvu Shooting.

Nionavyo mimi wote wananafasi ya kuzifungia timu zao kwa kuwa mifumo ya uchezaji wa timu inalenga kuwafanya wao ndiyo “main man” wafungaji, kifupi wanapasiwa mipira mingi ya aina zote na wachezaji kutoka idara ya kiungo. 

Hivyo very possible kupata magoli wote wawili kwenye mechi hii na kufanya mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora kuwa ng’adu ng’adu kwa wawili hao.

Basi wapwa zangu tumalize kwa home work hii, Binafsi yako unadhani nani atafunga goli leo, Fiston Kalala Mayele ama Reliant Lusajo!?.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.