Che Malone akimthibiti Jesus Moloko
Mabingwa Afrika

Yanga ni Rwanda na Simba Wao ni Zambia

Sambaza....

Rasmi Wananchi Yanga wamefuzu katika raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao saba kwa moja dhidi ya ASAS Djibout.

Upande wa pili kwa Simba wao tayari walishafuzu raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika bila kucheza mchezo wa awali kutokana na kuwa katika nafasi nzuri ya viwango vya vilabu Afrika.

 

Sasa wababe hao wa nchi wanaotokea Kariakoo wanakwenda katika vibarua vinavyofwata wakitafuta kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi hiyo Afrika.

Yanga wao baada ya kumpiga nyingi ASAS sasa wanakwenda kukutana na El-Merreck ya Sudan ambao wanachezea mechi zao za nyumbani nchini Rwanda katika uwanja wa kimataifa wa Huye kutokana na machafuko ya kisiasa ya nchini Sudan.

Wachezaji Yanga wakishangilia bao katika mchezo dhidi ya ASAS.

El Merreck wao wamefanikiwa kuvuka baada kupata matokeo ya jumla ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Othoho D’Oyo ya Congo Brazaville.

Yanga wataanzia ugenini Rwanda na kumalizia nyumbani. Wananchi pia wanakumbuka ambavyo mwaka jana walitolewa na Wasudan wenzao Al Hilal hivyo ni wakati wakulipa kisasi kwa Wasudan wenzao.

Simba iliyocheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa Simba wao watakutana na Power Dynamos kutoka Zambia ambao wamefanikiwa kupita kwa kuwatoa Wanamibia African Stars. Power Dynamos imepita kwa matokeo ya jumla ya sare ya mabao mawili kwa mawili. Ambapo walipoteza ugenini mbili kwa moja na kushinda bao moja sifuri nyumbani.

Michezo ya raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa inatarajiwa kupigwa kati ya September 15 na 16 wakati ile ya marudiano itapigwa kati ya September 29 na 30.

Sambaza....