Ligi Kuu

Yanga vs Singida, utamu wa mechi ulipo.

Sambaza....

Ligi Kuu Bara inaendelea kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Taifa jijini Dar és salaam, ambapo Yanga inayoshika nafasi ya pili  itaikaribisha Singida utd iliyopo nafasi ya tano katika ligi.

Mchezo wa kesho unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa pande zote kwa Yanga na Singida lakini pia na mashabiki wa Simba kwani mchezo huo unaamua pia hatma ya ubingwa wa SimbaSc.  Vitu vinavyofanya mchezo huo uwe na utamu wa aina yake:

TareheMwenyeji-MgeniUwanja

Vita Ya Ubingwa

Yanga wapo nyuma kwa alama sita nyuma ya vinara SimbaSc, Yanga ina alama 46 na SimbaSc wakiwa na alama 52. Hivyo kwa vyovyote vile Yanga wataingia uwanjani wakiwa na hamu ya kupata ushindi ili kupunguza alama na kubaki tatu ili Kuendelea kuipa presha Simba wanaongoza ligi. Kupoteza au sare kwa Yanga ina maana watakua wameanza kupotea katika mbio za ubingwa.

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC30209162154769
2Azam FC301610435161958
3Yanga SC301410644232152
4Tanzania Prisons30121262722548
5Singida Utd FC30111183028244

Yanga Haijawahi Kuifunga Singida.

Toka timu ya Singida utd ipande Ligi Kuu msimu baada ya kukosekana kwa zaidi ya miaka 10 haijawahi kufungwa na Yanga katika mechi za mashindano. Singida na Yanga zimekutana mara tatu mpaka sasa na Yanga kuambulia sare mbili na kipigo kimoja. Walikutana katika mchezo wa ligi raundi ya kwanza na kutoka bilabila, wakakutana katika Kombe la Mapinduzi wakatoka sare ya bao moja kwa moja, na mara ya tatu katika kombe lá  Azamsports FederationCup Yanga waliondolewa kwa matuta  baada ya sare ya bao moja kwa moja katika dakika 90.

Mchezo Wa Kisasi

Yanga wanaingia uwanjani katika mchezo na Singida utd kama kulipiza kisasi hivi mara baada ya kutolewa katika Azamsports FederationCup. Hivyo mchezo wa kesho utakua mahsusi kutaka kuwafunga ili kulipiza kutolewa katika kombe hilo.

Tiketi Ya Michuano Ya Kimataifa

Njia pekee ya Yanga kushiri michuano ya Kimataifa Africa mwakani ni kuchukua ubingwa wa ligi Kuu Bara، hii ni baada ya kutolewa katika Azamsports FederationCup hivyo kupoteza mbele ya Singida utd maana yake ni kuwaachia SimbaSc kujikita kileleni na kuuweka rehani ubingwa.

Mashabiki Wa SimbaSc

Huenda mashabiki wa SimbaSc wakawa wengi zaidi kesho katika uwanja wa Taifa kuliko wa Singida wenyewe wenye mechi. Hii ni kutokana na mchuano mkali wa kuwania ubingwa kati yao wawili. Hivyo Singida utd kesho watapata nguvu kubwa na support kutoka kwa mashabiki wa SimbaSc na kuwafanya wajisikie wapo nyumbani.

Kocha Wa Singida utd,  Plujim Hans

Hans van Plujim mkuu wa benchi la ufundi la Singida utd atakua akiiongoza timu yake dhidi ya waajiri wake wa zamani baada ya kupigwa chini Yanga na nafasi yake kupewa Lwandamina. Hivyo katika mchezo huo atataka kuwaonyesha walikosea kumuacha baada ya kuwapa taji la ligi Kuu Bara.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x