Tetesi

Yanga yamtaka SUREBOY

Sambaza....

Baada ya kuonekana kuzidiwa kete na Azam FC kwenye usajili wa kiungo wa zamani wa Kagera Sugar , Awesu Awesu , Yanga imeamua kuhamia kwa nahodha msaidizi wa Azam FC Abubakar Sureboy .

Kiungo huyo mshambuliaji amekuwa na timu ya Azam FC tangu daraja la kwanza mwaka 2008 mpaka msimu uliopita. Amedumu na Azam FC kwa muda wa miaka 12 na ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho.

Kiungo huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania amekuwa akiwaniwa kwa nguvu zote na mabingwa hao wa kihistoria nchini ili kuimarisha kikosi chao ambacho msimu uliopita kimefanya vibaya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.