Ligi

Yanga yavunja rekodi kibabe Iringa

Sambaza kwa marafiki....

Ile safari ya michezo 13 ya kucheza bila kupoteza mchezo iliyowekwa na Wajelajela Tanzania Prisons imefia mikononi mwa Yanga leo katika dimba la Samora mkoani Iringa.

Patrick Sibomana alitumia dakika 15 tu za mchezo kuweza kuwadhibiti askari hao magereza kwa bao safi, na bao lake hilo kudumu mpaka dakika ya mwisho ya mchezo. Kwa goli hilo sasa limehitimisha rekodi ya Tanzania Prisons ya kucheza ligi bila kupoteza mchezo wowote na kuipa alama tatu Yanga.

Patrick Sibomana mfungaji wa goli la ushindi la Yanga

Kwa matokeo hayo sasa Yanga imevuna alama 4 mkoani Mbeya na sasa wanajiandaa kuwavaa Biashara Utd jijini Dar kabla ya kuelekea January 4 kucheza na mtani wake Simba katika uwanja wa Taifa.

Mkwasa anaendelea kuuimarisha Yanga huku uchezahi wakikosi hicho ukionekana kuimarika na hivyo kupelekea mpambano wa Simba na Yanga kua mkali na wa kuvutia January 4.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.