Ligi Kuu

Yanga yawatolea tamko Kotei na Wawa

Sambaza....

Mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga, ulimalizika kwa sare tasa. Kama ilivyokawaida baada ya mchezo huu mkubwa hutokea menfi uwanjani na nje ya uwanja.

Katika matukio mengi yaliyojitokeza achilia mbali lile la Ibrahim Ajib kuanzisha mpira kwa kutoa nnje, mchezo huu ulikuwa faulo nyingi, ambazo nyingin zilipelekea mpira kuonekana mwamuzi kushindwa  kuumudu.

Tovuti ya kandanda ilifanikiwa kumpata Katibu wa matawi wa Yanga, Boazi amesema wanalaani kitendo cha mchezaji James Kotei na Pasacal Wawa kurusha masumbwi kwenye mchezo wa mpira wa miguu “Niwaombe kamati ya Waamuzi kupitia kwa makini video hizo (za tukio) na kuona jinsi ya kuchukua hatua sitahiki ili kulinda wachezaji na kukomesha vitendo hivyo vya kikatili.”

“Mchezaji Gadiel Michael alipigwa kwa makusudi na James Kotei huku refa akiwa karibu na tukio,pia Heriter Makambo alipigwa na Wawa wakingojea Kona ipigwe huku mwamuzi wa pembeni akiwa ameona na kujikausha naomba video ziangaliwe kwa uwazi na haki itendeke kama alivyo adhibiwa Obrey Chirwa msimu uliopita.” Alisisitza Boazi, ambae timu yake katika mchezo huo ilionekana kujilinda zaidi.

Hata hivyo, katibu alitoa pongezi kwa niaba ya matawi yote kwa wachezaji wote kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kujituma kwao kuilinda nembo ya klabu na kupata alama moja na kuendelea kuwa timu isiyofungika kirahisi.

Yanga hadi sasa imevuna alama 13 katika michezo 5 ya Ligi Kuu Tanzania bara hadi sasa.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x