Salum Aboubakar "Sure boy" akimtoka mchezaji wa Ruvu Shooting
Mashindano

Ajib hakuvutii vipi Sure boy na Hassan Dilunga kuachwa Stars?.

Sambaza....

Kama kigezo ni kucheza mpira nje ya nchi pasipo kuona mafanikio au matukio yao uwanjani basi ELIURD AMBOKILE alipaswa kuitwa na huyo Rashid Mandawa kuachwa.

Kocha AMUNIKE kama Ajibu hakuvutii na hana nafasi kwako, vipi kuhusiana na Hassan Dilunga na Sureboy??

Hivi kweli ukiangalia top scorers kwenye TPL utawaona wazawa wawili Salim Aiyee na Said Dilunga wakipambana na mapro kutafuta tuzo ya ufungaji bora.
Aiyee ndiye kinara mwenye magoli 13 wakati Said Dilunga ana magoli 10.
Ni ajabu kuona wachezaji hao kutoitwa timu ya taifa na badala yake tunawaita wakina Thomas Ulimwengu(hana kipya kwa Taifa) na Farid Mussa ambaye hana nafasi kabisa kwenye kikosi cha Teneriffe.

Amunike amerogwa na mapro wakati kuna wakali wapo hapa hapa bongo.

Anyway ngoja nifikirie hili la Abdi Banda kutoitwa na badala yake Ally Mtoni na Vincent Andrew!!

 

Junior Matukuta.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.