Ajib
Tetesi

Ajib hawezi kuchezea Yanga.

Sambaza....

 

Misimu miwili yenye mafanikio katika miguu ya Ibrahim Ajib iliwahi kutokea katika mitaa ya jangwani ambapo alifanikiwa kufanya vizuri sana katika klabu ya Yanga.

Baada ya kumaliza misimu yake miwili akiwa ndani ya klabu ya Yanga aliamua kurejea tena kwenye klabu yake ya zamani ambayo ni Simba Sc, mahasimu wakubwa wa klabu ya Yanga.

Ajib

Ingawa awali kabla ya kurudi Simba Sc, Ibrahim Ajib alikuwa anatakiwa na klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo lakini akaamua kuchagua kwenda Simba SC.

Alijiunga Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili na tayari ameshatumikia mwaka mmoja ndani ya mkataba wake wa miaka miwili mpaka sasa hivi hivo msimu ujao ndiyo utakuwa msimu ambao atamalizana na Simba SC.

Ibrahim Ajib

Mpaka sasa hivi kuna maswali mawili , la kwanza ni ufinyu wa namba katika kikosi cha Simba SC tangu ajiunge nayo na swali la pili ni timu ipi ambayo ataenda baada ya kumalizana na Simba SC .

Majibu ya maswali haya yamejibiwa na meneja wake. Ambaye amedai kuwa licha ya Ibrahim Ajib kukosa namba kwenye kikosi cha Simba SC lakini hawafikirii hata siku moja kumpeleka kwa mkopo Yanga SC au Azam FC.

“Hatuwezi kumpeleka Yanga SC au Azam FC kwa mkopo kwa sababu Ibrahim Ajib ana uwezo mkubwa wa kupigania namba kwenye kikosi cha Simba SC na tunaamini atafanikiwa kuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza”- alisema meneja huyo.

Pia kuhusu kumuuza Azam FC , Yanga SC au timu yoyote mara baada ya yeye kumalizana na Simba SC amedai kuwa Ibrahim Ajib hatocheza klabu ya hapa nchini tena ila baada ya kutoka Simba SC ataenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

“Kwa sasa Ibrahim Ajib hawezi kucheza tena kwenye timu za hapa nchini kwa sababu lengo letu ni yeye kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kwa sasa na siyo hapa nchini”- alimalizia meneja huyo wa Ibrahim Ajib.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.