Ligi Kuu

Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!

Sambaza....

Anaandika Ali Kamwe kwenye mambo 10!

1: 4G! MNARA UMESOMA KILELENI  YANGA IMESHINDA, MAYELE AMETETEMA. Ni usiku mwingine unaovutia kwenye kitanda cha kila Mwananchi!

2: NABI ametuma ujumbe wake mgumu kwenye kikosi. LENGO NI TIMU SIO MCHEZAJI BINAFSI. Ni kama ilivyokuwa kwa Conte na SON. Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.

3: Tactically, Sure Boy Ni PLAN B bora kwa Yanga kwenye mfumo wao. Kwa muda mrefu Yanga walikuwa na muundo wa 4-2-3-1 Lakini SURE BOY amempa NABI kiburi cha kwenda na 4-3-3! Kivipi?

4: Ubora wa SURE BOY kwenye kupiga
pasi sahihi/kwa haraka unaifanya Yanga iwe na muunganiko na Balance nzuri kwenye kushambulia.. What A Player! Direct Wingers wa Yanga [Ambundo/Moloko] wanaenjoy zaidi Mfumo huu kutokana na huduma wanayoipata katikati ya Uwanja.

 

5:MBEYA KWANZA wamehukumiwa na QUALITY. Ndani ya Uwanja na kwenye Benchi la Ufundi. Yanga walikuwa mbali mno. Kipindi cha kwanza ni kama walikuwa na aibu na kutoelewa nini kinaendelea uwanjani.. Yanga wakawaadhibu haraka haraka

6: Kipindi cha Pili Mbeya Kwanza waliamua kufunguka. Ni kama walikubali kucheza bila ‘Details’ nyingi vichwani. Wakaja kwenye TOTAL FOOTBALL. Bahati mbaya YANGA WALISHAMALIZA JAMBO LAO!

7: DIARRA NI JINI.. QUALITY. Bonge la Kipa. Sio kwa ajili ya kucheza tu na miguu.. Mikono yake iko imara pia. Ni mechi mfululizo sasa anafanya SAVES za Thamani kupambania Idadi ya CLEAN SHEETS ZAKE.

8: KUNA SURE BOY.. KUNA AUCHO! Utachagua kwa uelewa wako nani anastahili kuwa Man of The Match.. Miguuni mwao mpira ni mchezo rahisi sana! Ni ndoto ya mshambuliaji kucheza mbele ya kiungo mwenye jicho zuri la kuona nafasi na kupiga pasi sahihi

9: Habib Kiyombo.. Well Done! Lakini yule Hamis Kanduru ni kama alikuja kuweka sokoni kipaji chake.. What A Player! Alikimbia, alikokota, Alipiga kila alipopata nafasi. WENYE MACHO WAMEONA

10: Well Done Ambundo. Napenda kujiamini kwake kwenye maamuzi ndani ya Eneo la mwisho. Kazi nzuri Shomari Kibwana.. Lakini Farid Mussa anastahili heshima yake!

Nb: Walichobakiza ni Ubingwa wa kumshangilia Mpole

Sambaza....