Sambaza....

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam FC umewapa likizo wachezaji wake hadi Julai 3 mwaka huu ikiwa ni siku moja toka walipoifunga Yanga mabao 3-1 katika mchezo wa mwisho wa ligi siku ya Jumatatu Mei 28, 2018.

Akizungumza na wanahabari za michezo Japhary Idd Maganga amesema mbali na likizo hiyo, wamewapa wachezaji wao wagawane mapato ambayo yalipatikana katika mchezo wa Yanga kama asante kwa kufanya vizuri na kuwapatia nafasi ya pili msimu huu wa ligi.

“Kwanza tunashuruku matokeo ya jana dhidi ya Yanga, ulikuwa ni mchezo mzuri, tumepata nafasi ya pili ni heshima kwetu, mapato yote ambayo tumepata katika mchezo wa jana tumewapa wachezaji wagawane kwani wao ndio waliopambana,”

“Mbali na hayo tumewapatia wachezaji wetu likizo, tunatarajia kwamba kufikia tarehe 3-07-2018 tutarejea rasmi na pre season tutafanyia nchini Uganda kwa ajili ya kuiandaa timu, tunajua msimu ujao utakuwa msimu mgumu sana, kwa wachezaji wa Kimataifa tayari wameondoka kurudi makwao isipokuwa kwa Yahya Yakubu ambaye anaondoka leo usiku,” Maganga amesema.

Katika mchezo wa jana Mabao ya Azam yalifungwa na Yahya Zayd, Shaban Idd Chilunda na Salum Abubak ‘Sure Boy’ huku bao pekee la Yanga katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Taifa likiwekwa kimiani na Abdalah Kheri likiwa ni bao la kujifunga.

Sambaza....