Ligi Kuu

Beki Mwadui FC, aitamani Singida Utd

Sambaza....

Beki wa pembeni wa Mwadui FC, Miraji Makka amesema baada ya timu yake kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar, wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Singida United katika mchezo wa ligi Kuu bara utakaofanyika Jumamosi hii kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

Akizungumza na mtandao huu Makka ambaye aliwahi kuwika akiwa na Toto Africans ya Mwanza na Stand United ya Shinyanga amesema sababu kubwa ya kupoteza mchezo wao wa kwanza ilikuwa ni hujuma ya waamuzi kwani walionekena wazi kupendelea upande mmoja.

Mechi za Leo Jumamosi

“Tulipoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar lakini sababu kubwa ni kuwa wenzetu walijipanga vizuri nje ya uwanja, kama mchezo ungekuwa live ungejionea mwenyewe lakini hilo limepita na tunachoangalia kwa sasa ni mchezo uliyo mbele yetu dhidi ya Singida United” amesema.

Katika mchezo wa kwanza ambapo Makka alicheza dakika zote 90 Mwadui walipoteza kwa mabao 2-1 na wanaenda kucheza na Singida United ambayo nayo ilijeruhiwa na Biashara United kwa bao 1-0.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x