Ligi Kuu

Bernard Morrison ni majeruhi – NUGAZ

Sambaza....

Habari ya kwanza ilianza kwa Bernard Morrison kushindwa kusafiri na timu kwenda Shinyanga , na alipopigiwa simu kwa ajili ya kusafiri na timu hakupokea simu . Hofu ikazidi kupanda kwenye klabu ya Yanga .

Hofu zaidi ilizidi baada ya habari kuzagaa kuwa Bernard Morrison anatakiwa na mahasimu wakubwa wa Yanga , yani Simba . Habari ambazo zilianza kuwatia hofu kubwa sana Yanga.

Lakini mtandao huu wa Kandanda.co.tz na afisa uhamasishaji wa Yanga , Antonio Nugaz kuhusiana na ukweli wa Bernard Morrison. Antonio Nugaz aliuambia mtandao huu kuwa Bernard Morrison ni majeruhi.

“Alipata majeraha , ndiyo maana alishindwa kuhudhulia na timu kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga , lakini Bernard Morrison anaweza kwenda Dodoma kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania kama ataonekana anaweza kucheza”- alimalizia Antonio Nugaz


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.