Ligi Kuu

Bocco: Tikitaka zitakua nyingi kesho!

Sambaza....

Nahodha wa Wekundu wa Msimbazi Simbasc John Bocco ametuma salamu kwa Wanajeshi wa Mpakani Biashara fc kuelekea mchezo wao wa kesho katika mchezo wa raundi ya tatu ya muendelezo wa Ligi Kuu Bara.

Baada kukusanya alama nne ugenini na kufunga mabao mawili Simba inarudi katika uwanja wake wa nyumbani mbele ya mshabiki wake watapowakaribisha Biashara fc Jumapili saa moja kamili usiku.

Nahodha John Bocco amewaita mashabiki wa Simba huku pia akiahidi burudani yakutosha na  mabao mengi pia.

Ndemla na John Bocco

Bocco ” Niwakaribishe Wanasimba wote hapo kesho kwa burudani safi, tiki..taka zitakua nyinginyingi kabisa zikioongozwa na ushindi mnono inshaalah. Nguvu moja.”

Katika mchezo wa kesho Biashara United wanaingia uwanjani wakiwa hawajafungwa hata goli moja katika michezo yao miwili ya mwanzo, ambapo walipata ushindi wa bao moja dhidi ya Gwambina na Mwadui.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.