Ligi Kuu

CAF Yataja Waamuzi Wa Mechi Za Kimataifa Kwa Simba Na Yanga

Sambaza....

Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF limetoa orodha ya waamuzi watakaotumika katika hatua ya awali ya michezo ya Ligi Ya Mabingwa Barani Africa na Kombe La Shirikisho itakayopingwa kuanzia mwezi ujao. Kwa Tanzania itawakilishwa na vilabu Kongwe hapa nchini, YangaFC kwenye Klabu Bingwa na SimbaSC kwenye Kombe La Shirikisho.

Waamuzi kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF kuchezesha mchezo wa kombe la shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djibouti itakayochezwa Februari 22/02/2018 katika uwanja wa Taifa
Mwamuzi wa kati atakauwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja.

Abdallah Suleiman Gassim, mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Medir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi, Simon Samson na kamishina wa mchezo atatoka Botswana ni Mmonwagolthe Edwin Senai.

Wakati huo huo shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika CAF limewataja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Seychelles.

Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna wa mchezo atakuwa Frans Vatileni Mbidi

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x