Clatous Chama
Ligi Kuu

Chama bai baii Simba!

Sambaza....

Kiungo wa Simba Clatous Chama atakua nje kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mguu wake wa kulia.

Chama aliejiunga na Simba dirisha dogo akitokea RS Berkane ameumia kifundo cha mguu “enka” na ndio kilichopelekea kukosekana katika michezo dhidi ya Namungo na Ruvu Shooting.

Chama atakaa nje takribani wiki nne  na atakosa michezo minne dhidi ya Kagera Sugar, Azam fc, KMC na Geita Gold.

Kulikuwepo na tetesi kwamba Chama haelewani na benchi la ufundi na ndio sababu alikua haonekani kikosini, lakini mwenyewe alikiri kukosekana kwake ni kwasababu ya majeruhi na si vinginevyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.