Sambaza....

Klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga imefanikiwa kukiongozea nguvu kikosi chake baada ya kumrudisha mchezaji wao wa zamani Miraji Adam.

Coastal Union imefanya usajili huo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi na sasa Miraji Adam anakwenda kuungana na kina Bakari Mwamnyeto, Adeyum na Mbwana Kibacha katika eneo hilo.

Miraji Adam mchezaji wa zamani wa SimbaSc alikua akiichezea klabu ya Singida utd kabla ya kuvunja mkataba na kua mchezaji huru na kuamua kujiunga na klabu yake ya zamani ya Coastal Union aliyoitumikia kabla ya kushuka daraja mwaka 2016!

Miraji Adam maarafu na mtaalamu wa kupiga mipira iliyokufa na kubatizwa jina la “Mr Freekick”  mchezaji wa zamani ametambulishwa rasmi leo mbele ya waandishi wa habari jijini Tanga na kukabidhiwa jezi ya Coastal Union.

Sambaza....