Sambaza....

Kuna maeneo mengi sana ambayo hajaguswa kwenye mpira wa miguu hapa nchini kwetu. Ki msingi ni maeneo muhimu sana.

Na ni maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili tuendane na mapinduzi ya kisasa ya mpira wa mguu duniani.

Hapana shaka kwa sasa dunia inapitia mapinduzi makubwa sana ya kimbinu ndani ya uwanja. Mbinu nyingi sana zinatambulishwa.

Mifumo mingi sana inajaribiwa na makocha ili tu kuendana na mapinduzi ya kisasa ya mpira wa mguu duniani.

Uendeshwaji wa mpira umebadilika sana kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja. Ndiyo maana ukiingia ndani ya uwanja siyo ajabu ukamkosa mshambuliaji halisi wa kati.


[poll id=”3″]

Ni kitu cha kawaida sana kwa sababu hawa watu wameanza kupotezwa na mabadiliko ya kisasa kwenye mpira wa mguu.

Inawezekana kuna watu wengi husisitiza kuhusu uwekezaji wa kisasa kwenye vilabu vyetu ili kuendana na mazingora halisi ya sasa.

Inawezekana kuna watu wanatamani sana kuviona vilabu vyetu vikimiliki viwanja vyao vya kuchezea na kuachana na dhana ya kuomba viwanja vya watu.

Inawezekana kuna watu wanavisimanga sana vilabu vyetu kuhusu kutokuwa na viwanja vyao vya mazoezi (jambo ambalo ni la msingi).

Inawezekana kabisa kuna watu wanatumia muda wao kumwingi kuvishauri vilabu vyetu kutumia raslimali watu kwa ajili ya kupata wadhimini.

Inauma kuona klabu yenye raslimali watu wengi ikilia njaa, ni dhambi kubwa sana kwenye dunia hii ya kibiashara. Dunia ambayo wafanyabiashara wanatafuta sehemu nzuri ya kutangaza bidhaa zao.

Dunia ambayo siyo rahisi kwa mfanyabiashara kuwekeza sehemu ambayo ina watu wengi kwa kujua kabisa atanufaika sana.

Yote haya yanazungumzwa kwa nia njema sana, nia ya kujenga. Hakuna ambaye anatamani kuendelea kuviona vilabu vyetu vikiwa katika hali ya umasikini.

Hakuna anayetamani kuviona vilabu vyetu vikishindwa kushindana na vilabu vikubwa barani Afrika kwenye mashindano ya Afrika.

Ndiyo maana wengi wetu hutumia muda wengi mwingi kuwakumbusha njia wanayotakiwa kupitia viongozi ambao tuliwapa dhamana ya kutuongoza.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho tumekisahau sana siku hizi. Kuna eneo ambalo hatuligusi sana na ni eneo ambalo ni muhimu sana.

Wachezaji wengi hawana wasimamizi wa kazi zao. Wasimamizi ambao wanauwezo wa kuwashauri na kuhakikisha wachezaji wanatumikia vipaji vyao ipasavyo.

Wasimamizi ambao watawakumbusha wachezaji muda wa kufanya mazoezi binafsi. Muda wa kwenda kula na muda sahihi wa kupumzika.

Jonas Mkude akishangilia

Wasimamizi ambao watahakikisha mchezaji asitumie chochote kitu ambacho kitamdhuru mfano pombe.

Wasimamizi ambao watamkumbusha mchezaji uchaguzi wa maneno ya kuongea mbele ya vyombo vya habari ili kuilinda sura yake kibiashara.

Wasimamizi ambao watamuonesha mchezaji kuwa yeye ni nembo ya kibiashara hivo anatakiwa kujilinda ili ailinde biashara yake.

Wasimamizi ambao watahakikisha wanamjenga kisaikolojia mchezaji kipindi ambacho amekubwa na kitu ambacho kinaweza kumbomoa.

Hiki ndicho kilichonifanya nimkumbuke Jonas Mkude. Aliwahi kuporowa kitambaa cha unahodha. Kitu kiuhalisia kinaweza kumshusha mchezaji.

Mwanzoni alikuwa ametetereka lakini kadri siku zinavyozidi kwenda anaimarika. Inawezekana Jonas Mkude alipata mshauri mzuri wa kumjenga.

Jambo ambalo ni jema sana, ni jambo ambalo tunatakiwa kulifanyia uwekezaji mkubwa kwa wachezaji wetu kwa sababu tu huwa wanapitia magumu mengi ambayo huwafanya kuwahitaji watu wa kuwajenga.

Hili ni eneo muhimu sana ambalo tunatakiwa kuliwekeza kwenye mpira wetu. Tunaweza tukawa tunawaza kuwekeza viwanja.

Tukawaza kuwekeza timu za vijana. Mambo ambayo kimsingi ni muhimu sana kwenye maendelo ya mpira wetu.

Lakini tukasahau sehemu moja ambayo ni muhimu sana. Sehemu ya chakula cha akili cha mchezaji. Kuna wakati wachezaji akili zao hutingwa.

Ndiyo wakati ambao huitaji watu wenye funguo za kufungua mazito ambao huwa wanatingwa nayo kwa kuwalisha chakula cha akili, chakula ambacho huwaimarisha vizuri.

Sambaza....