Ligi Kuu

GSM yamwaga hela chafu kwa kina Nchimbi!

Sambaza....

Leo ligi kuu ya Tanzania bara inaendelea baada ya likizo ya Corona. Leo michezo miwili itachezwa katika mikoa miwili tofauti , mkoank Tanga nyumbani kwa Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani kutakuwepo na mchezo mmoja.

Mchezo mwingine utakuwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambapo Mwadui FC watakuwa wenyeji wa mabingwa wa kihistoria Yanga ambao wamesafiri moja kwa moja kutoka Dar es Salaam.

Ditram Nchimbi (Kushoto) wa Yanga akiwania mpira mbele ya Juma Nyosso (Kulia).

Katika mchezo huu wadhamini wao GSM wameahidi pesa kwa wachezaji wa Yanga kama watafanikiwa kuifanya Mwadui FC kwenye mchezo huo , ahadi hiyo imetolewa kwenye kikao cha jana jioni kati ya GSM , uongozi wa Yanga na wachezaji wa Yanga kilichofanyika kwenye uwanja CCM Kambarage.

Kabla ya ligi kusimama kwa sababu ya ugonjwa wa Corona , kampeni ya GSM ilikuwa inatoa kiasi cha milioni 10 kwa wachezaji  kwa kila mechi ambayo Yanga walikuwa wanashinda ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza motisha kwa wachezaji.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.