Ligi Kuu

Habari za hivi punde: Mayanga wa Taifa Stars atua Mbao FC.

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Mbao ya jijini Mwanza kupitia ukurasa wake wa Instagram imemtangaza kocha Salum Mayanga kuwa kocha wake mkuu ikiwa ni siku chache baada ya kumtimua Kocha Ally Bushiri aliyekuwa akishikilia mikoba hiyo.

Kabla ya kibarua hicho, Mayanga alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa mabingwa wa kombe la FA Mtibwa Sugar lakini pia amewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) pamoja na vilabu mbalimbali vikiwemo Tanzania Prisons pamoja na Mtibwa Sugar yenyewe.

Taarifa zaidi itafuata:

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.