Ligi Kuu

Hajji Manara: Simba ni kama Liverpool

Sambaza....

Msemaji wa Klabu ya soka ya Simba Sports Club Hajji Manara ametoa kali baada ya kuifananisha klabu yake na wababe wa EPL majogoo wa  Liverpool.

Hajji Manara ameyasema hayo alipokua akihojiwa na Maulid wa Kitenge katika mahojiano na redio ya Wasafi fm.

Hajji Manara “Sisi Simba tuna ligi yetu halafu wao timu zingine wana ligi yao kama ambavyo Liverpool wanafanya pale Englanda. Kuna Yanga na hao Singida, Ruvu Shooting na Kagera wana ligi yao sisi tupo huku juu tunatafuta ubingwa.

Tunaongoza kwa alama 16 ili Yanga atufikie tunatakiwa tupoteze michezo mitano, sasa Sheikh Simba hii inafungwaje michezo mitano? Tutakua wapi? Au tutakua tumelewa au tumelala?”

Hajji pia aliongeza ” Simba hii yenye Wawa, Nyoni, Kotei, Bocco na Kagere huwezi ifunga michezo mitano, labda tutapoteza mchezo mmoja lakini si mitano.

Sikumbuki mara ya mwisho lini Simba imefungwa mabao matatu tena katika uwanja wa nyumbani pale Taifa.”

Mpaka sasa katika Ligi Kuu nchini Uingereza  EPL  Liverpool ndio kinara wa ligi hiyo akiwa anaongoza kwa tofauti ya alama 16 na mtu anaemfwatia Manchester City wanaoshika nafasi ya pili.

 

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.