Ligi Kuu

Hawa hapa watakaoamua mchezo kati ya Yanga na Simba.!

Sambaza kwa marafiki....

Kuelekea mchezo namba 260 wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga atakua mwenyeji wa Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tayari shirikisho la miguu nchini limetaja waamuzi watakaoamua mchezo huo.

TFF leo wamewataja waamuzi hao kutoka mikoa ya Morogoro, Tanga, Singida na Dar es salaam. Huku wengi wao wakiwa ni waamuzi wazoefu wakiwa wameshashiriki katika  kuchezesha michezo hiyo ya Simba na Yanga.

Mwamuzi wa kati ni  Martin Saanya (Morogoro), mwamuzi msaidizi namba moja ni Mohamed Mkono (Tanga), mwamuzi msaidizi namba mbili ni Frank Komba (Dar es salaam) na mwamuzi wa akiba ni Elly Sassii wa Dar es salaam.

Pia waamuzi wa ziada watakua ni Abdallah Mwinyimkuu (Singida) na Ramma Kayoyo (Dar es salaam) na mechi kamishina Mohamed Mkweche.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.