Ligi Kuu

Ibrahim Ajib ni yule yulee tuu!

Sambaza kwa marafiki....

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu amekua na kiwango kizuri msimu huu kiasi cha kufanya mashabiki wa Yanga kupagawa na kiwango chake tangu mwanzo wa msimu.

Ajib chini ya mwalimu Zahera aliuanza msimu wa mwaka 2018/2019 kwa kasi ya hali ya juu akitoa pasi za mabao ama kuamua kufunga yeye mwenyewe. Kwa kiasi kikubwa kutokana na magoli yake na “assist” aliweza kuiongoza Yanga sc kucheza michezo 15 bila kupoteza.
Lakini tangu msimu ulipofika kwenye hatua za lala salama Ibrahim Ajib amekua sio Ajibu yule alieanza kwa kasi mwanzoni mwa msimu.

Ibrahim Ajib “Cadabra”

Haishangazi kumuona Ajibu akiwa benchi kama mchezaji wa akiba na hii ni kutokana na uwezo wake kupungua kwa hali ya juu.
Ibrahim Ajib kwanza alianza kwa kufanyiwa mabadiliko hivyo kushindwa kumaliza dakika 90 lakini sasa anaanzia benchi kabisa. Kwenye michezo minne mfululizo amekua akitolewa, kwenye michezo ya Yanga vs Simba, Namungo vs Yanga, Jkt vs Yanga na Singida vs Yanga (alianzia benchi). Lakini katika mchezo wa Allince School alianzia benchi na kutokucheza kabisa.

Kwenye michezo 10 ya kwanza Ibrahim Ajib aliweza kutoa msaada wa mabao “assist” 13 lakini kwenye michezo mitano ya mwisho ametoa “assist” moja tu.

Ibrahim Ajib ni yule yulee tuu anaeanza Ligi akiwa wamoto na kadri Ligi inavyozidi kuchanganya ndivyo nayeye anavyozidi kupotea.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.