Habibu Haji Kyombo akitambulishwa na Simba.
Uhamisho

Iwe Kitaifa au Kimataifa atatoboaa!

Sambaza....

Achana na mtizamo wa mashabiki wa soka hasa wa Simba juu ya ujio wa mshambuliaji mzawa Habib Kyombo ndani ya kikosi hicho na ‘ attention’ walioiweka kwenye utambulisho wake.

Kwa haraka niseme upinzani wa Simba na Yanga hasa kwenye kutambulisha ‘vipuri’ vyao katika kipindi hichi cha usajili ndiyo kumesababisa maoni tofauti juu ya ujio wa Kyombo.

Basi siye tumtizame kwenye angle ya kiufundi kyombo ni mchezaji gani na anaweza kuifanyia nini Simba inayotaka kurejesha ubingwa wake waliporwa na wapinzani wao wakubwa Yanga katika msimu huu.

Habib Kyombo ni mchezaji kijana mwenye umbo zuri ( body Morphology) kwa nafasi anayocheza ya ushambuliaji wa kati.

Tunaposema umbo zuri tunaangalia kimo chake ambacho ni futi 6 na ushee na kujengeka kimichezo,ambapo faida ya moja kwa moja ni matumizi ya mipira ya juu ikiwemo kufunga kwa kichwa.

Umri wake wa chini ya miaka 23 akiwa na umri wa miaka 21 kwa sasa ( ni mzaliwa wa 12/Dec/2000 inatoa tafsiri ya moja kwa moja kuwa na nguvu kwa support ya umri ( age hii mara nyingi huwa mwili na akili huwa active sana) na hapo ndiyo kwanza hajafika kupevuka kisoka ( maturity) inayoanzia 23-29.

Intelligence Quality ( I Q) ni kubwa sana hapa tuna maana ya kipaji kwa ujumla na matumizi makubwa ya akili michezo ndiyo maana utakubaliana nami tangu anacheza Mbao alionesha yeye ni mchezaji wa aina gani maana kipaji hakifichiki angalia goli alilowafunga KMC something like rabona.

Uwezo wake wa kufunga hapa ndipo utambulisho halisi wa Kyombo ulipo ni fundi wa kufunga kwa mifumo yote iliyopo uwanja anafunga kwa kichwa ,miguu yote kulia na kushoto waweza kusema ana footwork nzuri ,lakini pia anafufua mipira iliyokufa kitu ambacho ni faida sana ukiwa na mchezaji wa aina hii kwenye timu hii inawezakuthibitishwa pia na tuzo ya ufungaji bora aliyowahi kuipata akiwa na Mbao kwenye Azam Sports Federation Cup.

Pia ukimuangalia alivyojiunga na Mbeya kwanza January mwaka huu ameitumikia Mbeya kwanza michezo 12 na kuwafungia magoli 6 na kuassist mara kadhaa akiwa amecheza dk 1054 hapa unaweza kujua ni mshabuliaji wa aina gani.

Exposure na experience yake kitaifa na kimataifa ni kigezo kingine kinachoweza kumfanya afanikiwe ndani ya Simba kucheza professional league huongeza kitu kikubwa sana sana kwa mchezaji yeyote yule duniani.

Licha ya kutokupata nafasi kwenye Senior team ya Mamelod Sundowns kule alipopelekwa kwa mkopo TS sporting amefanikiwa kuongeza maarifa zaidi.

Hivyo anachokwenda kukiongeza kwa kaka zake pale Simba ni number of goals , mapambano physical battle’ kutokana na ‘play style yake’ kujitegemea na kutegemea wenzake ukilinganisha changamoto wanazopitia washambuliaji waliopo Mugalu ,Kagere na Bocco.

Anakwenda kuadd kitu kikubwa ndani ya wekundu wa Msimbazi Simba Sport kwa faida nyingi tu ikiwemo umri huo endapo anapata majeraha ni rahisi kulicover hivyo kuna mategemeo ya kuwepo mara kwa mara mchezoni.

Akijengwa vizuri kisaikolojia pia kwa kucheza Simba msimu huu ni platform ya kuonekana tena kurejea kwenye masoko mengine makubwa ya Africa ikiwezekana nje ya bara la Africa.

Na Simba wakapata fedha nyingi kwa mauzo yake endapo atashine na kuhitajika kwenye timu nyingine.

Sambaza....