Ligi Kuu

Jinsi Yanga walivyobadili msimamo!

Sambaza....

Wana Jangwani baada ya kufanikiwa kuwafunga Kagera Sugar bao moja kwa sifuri katika dimba lao la Kaitaba Bukoba sasa wamesogea juu na kushika nafasi ya kwanza na kuwaacha KMC,Biasahara, Dodoma Jiji pamoja na Azamfc walioshinda michezo miwili kufuata chini yake.

Ni Mukoko Tonombe ndie aliepelekea furaha Jangwani baada ya makosa yaliyofanywa na Ally Sonso kushindwa kumzuia Tuisila Kisinda aliepita kwa kasi na kupiga mtungi ndani uliotumiwa vyema na Mukoko, Yanga wenyewe wanakwambia “Made in Congo”.

Mukoko Tonombe

Matokeo mengine jana Prisons walifanikiwa kuifunga Namungo bao moja kwa sifuri wakicheza kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wao wa Rukwa katika dimba la Nelson Mandela.

Tazama hapa msimamo

Msimao wa Ligi Kuu Bara

PosTimuPWDLGDPts
13426536483
234211123174
334191142868
434131110-450
534139121248
63410159245
734101410044
834111112-344
934101311-743
103411815-441

Ligi Kuu Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu pia ambapo Mbeya city wataikaribisha Azamfc wakati Coastal Union itakua nyumbani kutafuta ushindi wake wa kwanza mbele ya Dodoma jiji na Simbasc watakua na kibarua mbele ya Biashara Utd kwa Mkapa.

Mzunguko wa tatu utakwenda kuhitimishwa kesho na Mwadui fc watakaowakaribisha KMC “Kino Boys” katika dimba la Mwadui Complex.

Sambaza....