Ligi Kuu

John Mbisse: Tunashukuru serikali kusimamisha Ligi.

Sambaza....

Kiungo wa Namungo Fc “The Southern Killers” ambayo inafanya vizuri kwasasa katika Ligi Kuu Bara ametoa maoni yake kuhusu ugonjwa wa corona na pia kusimama kwa Ligi kutokana na agizo la Waziri Mkuu la kusitisha michezo ya ligi mbalimbali ili kupunguza mikusanyiko ya watu.

Kiungo huyo wa zamani wa Simba, Dodoma fc na Friends Rangers amesema serikali imefanya jambo sahihi kusimamisha Ligi lakini pia kama timu wanaweza kutumia kipindi hiki kufanya marekebisho ya makosa yao.

John Mbisse “Mimi kama mchezaji kwanza ningependa kuwapongeza serikali kwa kuchukua uamuzi wa kusimamisha Ligi (VPL) maana ugonjwa wa corona ungeweza kuwaathiri watu wengi kwa urahisi sana. Kama ambavyo tunavyojua watu wengi wanapenda mchezo wa mpira mpira wa miguu  hivyo ingewezekana watu wengi kupata maambukizi kwa haraka zaidi na ingeleta janga kubwa zaidi kwenye Taifa letu.

John Mbisse kiungo wa Namungo Fc.

Ila kuhusu timu nadhani inawezekana wakatumia wakati huu wa Ligi kusimamishwa kurekebisha makosa yao ili kuzipa timu zao nguvu zaidi nje ya uwanja maana sidhani kama timu zinaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa sana baada kusimamishwa kwa ligi kwa mtazamo wangu mimi kama mchezaji”

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na kiungo mkabaji kwa ufasaha kabisa  pia amezungumzia unafuu wanaoupata baada ya Ligi kusimama na nafasi ya nafasi yao katika Ligi haswa katika swala la wachezaji kuchoka kutokana na ratiba ngumu na usafiri, lakini pia kujitunza kama mchezaji baada ya ligi kusimama.

John Mbise “Kwenye maswala ya kujilinda kama mchezaji ni kujitambua wewe kama mchezaji na kuishi katika miiko ya mpira. Lakini pia katika  kuwania nafasi  za juu katika Ligi sio jambo rahisi kama ligi ingeendelea maana wachezaji walikuwa hawapati muda wa kupumzika sababu kila baada ya siku tatu mechi lakini pia ukizingatia usafiri wa timu nyingi ni tatizo naimani haya mapumziko yatazisaidia timu zote za VPL na sio sisi tu Nàmungo pekee.”

 

Sambaza....