Blog

Juma Mahadhi arejea kumpiga benchi Morrison !

Sambaza....

Unaikumbuka mechi kati ya Yanga SC na TP Mazembe pale uwanja wa Taifa ? Mechi ambayo tajiri na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo , Yusuph Manji alipoamua kuwalipia mashabiki wa Yanga kiingilio na wakaingia bure.

Tuachane na mambo ya kiingilio kwenye hiyo mechi. Kuna kitu kimoja tu ambacho huwa kinakuja kila nikikumbuka hiyo mechi , kitu chenyewe ni kiwango kikubwa cha Juma Mahadhi. Nakumbuka alivyokuwa amenyoa , nakumbuka mpaka njumu alizokuwa amevaa.

Nakumbuka vyote hivi kwa sababu ya kiwango chake kikubwa kwenye mechi ile. Baada ya ile mechi sijawahi kumuona tena Juma Mahadhi akicheza kwenye kiwango kile kikubwa. Na kwa bahati mbaya majeraha yakamweka nje ya uwanja tena.

Kuelekea kuanza tena kwa ligi kuu ya Tanzania bara , daktari wa Yanga amedhibitisha kuwa Juma Mahadhi amerejea tena kwenye klabu hiyo baada ya kupona majeraha yake ambayo yalikuwa yanamsumbua muda mrefu.

“Juma Mahadhi kashapona majeraha yake , yuko tayari kuungana na kikosi chake tena na kwa sasa anafanya mazoezi ambayo yanatokana na programu ya mwalimu” alisema daktari Ngazija , daktari wa Yanga.

Urejeo wa Juma Mahadhi unakuja na swali kubwa la namna ambavyo anaweza kugombania namba na Bernard Morrison ambaye kwa sasa anaonekana ni nyota wa kikosi cha Yanga.

Sambaza....