Tetesi

Kagere na Mkude hawaendi kokote -Manara

Sambaza....

 

Kumekuwa na taarifa nyingi sana ambazo kuhusu baadhi ya wachezaji wa klabu ya Simba kuondoka Simba na kwenda kujiunga katika vilabu mbalimbali ndani na nje ya nchi .

Hivi karibuni kulikuwepo na taarifa ya mshambuliaji hatari wa Simba , Meddie Kagere kutakiwa na vilabu mbalimbali nchini Hispania . Taarifa ambayo iliripotiwa na kituo kimoja kikubwa cha habari hapa Tanzania.

Taarifa za wachezaji nyota wa klabu ya Simba kutakiwa na baadhi ya timu zimekuwa kama taarifa ambazo ni mkuki wa moto kwenye mioyo yao kwa sababu wachezaji hawa ni vipenzi na tegemeo kubwa sana katika timu ya Simba kwa sasa ndiyo maana mashabiki wengi wa Simba wamekuwa wakiingiwa na hofu kubwa.

Kuwaondoa hofu hiyo , Afisa habari wa klabu ya Simba , Haji Manara amewatoa wasiwasi kuwa wachezaji hawa hawatoenda popote wakati huu ambao tunasubiri ligi ianze tena baada ya kusimama kutokana na janga la Covid-19.

Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba

Haji Manara ameanza kwa kusema kuwa mpaka sasa hivi hakuna ofa yoyote iyokuja kwenye meza ya Simba kutoka kwenye vilabu mbalimbali kuwahitaji hao wachezaji ambao wanatajwa sana.
“Hakuna ofa iliyokuja mezani kuwahitaji Jonas Mkude na Meddie Kagere mpaka sasa hivi”.

Moja ya mikutano ambavyo timu inaweza kutangaza viingilio au utaratibu wa mapato yao. Pichani ni Haji Manara, Msemaji wa Simba SC.

Haji Manara akaongeza kuwa Simba kwa sasa ni klabu kubwa sana inautaratibu maalumu wa kutoa taarifa zake. “Simba ni klabu kubwa sana , ina utaratibu wake wa kutoa taarifa zake na haiwezi kutoa taarifa kienyeji enyeji tu , kwanza hizo taarifa nimezisikia kwako”- alisema Afisa habari huyo wa Simba. Kuna habari zinaenea Jonas Mkude anahitajika na Tp Mazembe wakati Meddie Kagere anahitajika na Levante ya Hispania.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.