John Mbisse kiungo wa Namungo fc.
Ligi Kuu

Kiungo Namungo anaitaka Ligi kwa hamu!

Sambaza....

Kiungo wa klabu ya soka ya Namungo fc John Mbisse amesema wao kama Namungo wako tayari kwa Ligi kurudi kama kawaida huku wakiitangazia vita klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga.

John Mbisse ” Tayari wote tupo kambini na tunaendelea na mazoezi ya nguvu kama kawaida chini ya walimu wetu wote.
Kwa jinsi hali ilivyo  mpaka siku ya mchezo tutakua tupo vizuri kabisa.

John Mbisse akiwa mazoezini na kikosi cha Namungo!

Mbisse mchezaji wa zamani wa Simba na Dodoma fc  pia amezungumzia hali yake ya utimamu wa mwili baada ya kukaa kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu.

“Kwasasa nimepona kabisa nipo fiti, nilikaa njee kwa muda mrefu kutokana na kuuguza kifundo cha mguu ndio maana nilikua sijaonekana na timu muda mrefu.
Lakini kwasasa niko tayari kuitumikia timu yangu nasubiri tuu mwalimu anitumie kikosini.” John Mbisse.

Namungo Fc itacheza mchezo wake wa kwanza baada ya Ligi kurudi dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga. Tayari Namungo wamesema hawapo tayari kupoteza alama zote sita mbele ya Wagosi wa Kaya. Coastal Union ndio klabu ya kwanza kuifunga Namungo katika uwanja wake wa nyumbani msimu huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.