Tetesi

Kiungo Prisons: Yanga ni kama nyumbani.

Sambaza....

Kiungo kinda wa Tanzania Prisons Cleophace Mkandala amewaka wazi Yanga ni nyumbani na yupo tayari kwa wakati wowote kurudi kwasababu aliondoka pale vizuri na ndio klabu iliyomkuza.

Mkandala alipitia kikosi cha vijana cha Yanga kabla ya kuondoka baada ya kukosa nafasi ya kupandishwa katika kikosi cha wakubwa. Baada ya kutimka Yanga alienda katika kikosi cha Tanzania Prisons ambapo amefanya vizuri na Wajelajela hao kiasi cha kupelekea klabu yake ya zamani kutaka kumrudisha tena.

Akizungumzia hatma yake kipindi dirisha la usajili litakapofunguliwa amesema Yanga ni nyumbani.

Cleophace Mkandala wa Tanzania Prisons akizungukwa na wachezaji wa Yanga Raphael Daud, Ibrahim Ajib na Feisal Salum.

Mkandala “Yanga ni kama nyumbani kwangu maana nilipita pale katika timu ya vijana hivyo sina shida ya kurejea tena pale. Kwa upande mwingine itakua ni vizuri mimi kujunga tena na wao.

Ni jambo zuri kuhusishwa na klabu yangu ya zamani kwa maana wameona kazi nzuri niliyoifanya nikiwa  na Prisons”

Kiungo huyo ambae anamudu kucheza kama mlinzi wa kulia pia amedokeza endapo atahitajika na klabu nyingine nje ya Yanga kama yupo tayari.

Cleophace Mkandala.

“Mpira ni kazi yangu hata timu nyingine kama zitanihitaji nipo tayari kwenda kuzitumikia na kufanya nao kazi.

Lakini nina malengo makubwa zaidi ya kucheza soka nje ya nchi hiyo ndo ndoti yangu, haina kufeli kama brother Samatta.” Mkandala.

Cleophace Mkandala pia amesema alifurahu alipoitwa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza na hakuacha kumsifia mwalimu wa timu ya Taifa na kusema ni mwalimu mzuri ambae anajua kukuza vipaji vya vijana wadogo.

Sambaza....