Novatus Dismas
Uhamisho

Kiungo wa Stars asajiliwa Ubelgiji!

Sambaza....

Kiungo wa ulinzi wa Timu ya Taifa ya Tanzania Novatus Dismas amefanikiwa kusajiliwa na klabu ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji na kuachana na Makabi Tel Aviv ya nchini Israel.

Novatus mchezaji wa zamani wa Azam Fc na Biashara United amejiunga na Zulte Waregen kwa mkataba wa miaka mitatu na sasa atakua akionekana katika Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiter Pro League

Novatus Dismas katikati akisaini kuitumikia klabu yake mpya ya Zulte Waregen akiwa na wasimamizi wake Ibrahim Mohamed na Shaffih Dauda pamoja na viongozi wa klabu hiyo.

Novatus 19, alikua akiitumikia Makabi Tel Aviv ya Israel akitokea Azam Fc  baada yakipandishwa kutokea timu za vijana.

Kiungo huyo wa ulinzi amekua sehemu muhimu katika kikosi cha Stars kwasasa chini ya kocha Kim Polsen.

Novatus sasa anafwata nyayo za nahodha wake wa Taifa Stars Mbwana Sammata ambae alicheza kwa mafanikio nchini hapo akiwa na klabu ya KRC Genk.

Novatus hatokua pekeake katika Ligi hiyo na nchi hiyo kwa pia yupo kinda Kelvin John anaeitumikia KRC Genk ya vijana walio chini ya miaka 20


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.