Sambaza....

Wananchi Yanga rasmi kesho wanaanza kutetea taji lao la Ligi Kuu ya NBC watakapovaana na KMC Fc katika mchezo wao wakwanza wa Ligi.

Yanga watakua nyumbani katika uwanja wa Azam Complex na watawakaribisha KMC majira ya saa moja kamili usiku.

 

Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema “Ratiba  kweli ni ngumu kutokana na ratiba ya michezo kuwa mingi lakini hiyo ndio kazi yetu,” alisema na kuongeza;

“Tunapaswa kujiandaa kama timu kubwa ili kupata matokeo chanya katika kila mechi.”

Gamondi pia ameelezea hali ya majeruhi kuelekea mchezo wa kesho, huku pia akitanabaisha ameandaa timu vyema kwaajili yakutoa burudani kwa Wananchi.

Yao.

“Tulikuwa na shida kwa wachezaji kadhaa, tutawaangalia kwenye mazoezi ya leo mchana kuona kama tunaweza kuwatumia kesho. Lakini kiujumla afya za wachezaji wetu ipo imara na wana utayari wa kucheza mchezo wa kesho.”

“Nawasihi mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kesho. Tutacheza kandanda safi na la kuvutia ili tupate matokeo. Tupo kwenye njia sahihi, tumejipanga na tumejiandaa kuwapa buduruni,” alimalizia Gomondi.

Nae winga wa pembeni Denis Nkane amesema wao kama wachezaji wapo tayari kutetea taji lao na wanawaita mashabiki wajee kwawingi kesho Chamazi.

Denis Nkane.

“Jambo la thamani kwetu ni kucheza mbele ya mashabiki wetu kwa sababu wao ndio wamekuwa chanzo cha hamasa ya ushindi wetu. Uwepo wao uwanjani ni chachu ya ushindi, tunawasihi sana wajitokeze kwa wingi.”

“Tumempokea vizuri mwalimu na kila Mchezaji anapambana kuonesha kitu ili aingie kwenye mfumo wa mwalimu. Lengo kuu la Klabu yetu ni mataji si vinginevyo, jambo la kuzingatia kushinda mechi zote muhimu kutimiza hilo.”

 

Sambaza....